Michael Owen astaafu

Image caption Michael Owen astaafu

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England,Michael Owen ametangaza kutundika daruga ama kupumzika kucheza soka la ushindani mwishoni mwa msimu huu.

Hii imekuwa ni ghafla,lakini wachambuzi wengi wa soka na mashabiki wa mchezo huo ulimwenguni walitarajia taarifa hii.

Owen mwenye umri wa miaka 33,aliifungia England mabao 40 katika michezo 89 aliyoichezea timu hiyo ya taifa,Alianza soka lake akiwa kwenye klabu ya Liverpool alikopata mafanikio makubwa kabla ya kuhamia Real Madrid ya hispania na kisha kurejea Uingereza na kujiunga na klabu ya Newcastle,baadaye alijiunga na Manchester United kabla ya kuhamia Stoke City ambako anacheza hadi hivi chini ya mkataba maalumu.

Michael Owen amesema anashukuru kuona taaluma yangu ya mpira wa miguu imenifikisha sehemu ambapo nilikuwa nikiota kupafikia.

Michael Alianzia wapi?

Alianza kuwika akiwa na kikosi cha Liverpool na dunia ilimtambua zaidi kwenye miaka ya 1998 akiwa na umri wa miaka 18 wakati alipoitwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki kombe la Dunia mwaka huo na bao lake la pekee dhidi ya Argentina kwenye michuano hiyo lilimpa umaarufu zaidi kabla ya kufunga mabao matatu peke yake maarufu kama hat trick katika mechi ambayo England iliwafunga Ujerumani kwa mabao 5-1 mwezi Septemba mwaka 2001.

Hadi hivi sasa Owen amekwisha funga jumla ya magoli 220 kwenye klabu alizochezea,Huku akitwaa Mataji ya Ligi kuu soka nchini England,Kombe la FA,Kombe la Ligi mara tatu na kombe la Uefa.

Image caption Michael Owen astaafu

Mwaka 2001,Owen alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya,akiwa ni Muingereza wa kwanza kutwaa tuzo hiyo baada ya Kevin Keegan aliyetwaa kwenye miaka ya 1976.

Mwaka 2005,Owen alipata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu wake akiwa anaichezea timu yake ya taifa,Toka hapo amekuwa ni mwenye kusumbuliwa na majereha ya mara kwa mara.

Toka amejiunga na timu yake ya sasa ya Stoke City,Owen amekwisha funga bao moja tu katika michezo saba aliyoichezea timu hiyo.

Michael Owen,amezishukuru klabu zake zote alizowahi kuchezea pamoja na mashabiki wake toka akiwa Liverpool mpaka sasa Stoke ambapo amesema kwa sasa hana tena miaka 18 na hana budi kuachana na soka la ushindani,aliandika katika mtandao wake.

Pamoja na yote,Owen atandelea kukumbukwa na waingereza wote kutokana na kipaji chake pamoja na bao lake pekee na la muhimu katika michuano ya kombe la dunia dhidi ya Argentina.