Bayern kukwaruzana na Barcelona

Wachezaji wa Bayern Munich
Image caption Wachezaji wa Bayern Munich

Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes, amesema atawashirikisha wachezaji wake wote katika mechi ya raundi ya nusu fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya leo usiku, dhidi ya Barcelona.

Hata hivyo kocha huyo amesema uamuzi huo ni kutokana na azma yao ya kufuzu kwa fainali licha ya kuwa wachezaji wake sita wa kutegemewa wanakabiliwa na tishio la kukosa mechi ya fainali, ikiwa watapewa kadi nyingine ya njana, endapo watafuzu kwa fainali hiyo.

Katika mechi ya awamu ya kwanza Bayern iliinyuka Barcelona kwa magoli manne kwa yao. Amesema wachezaji wake wanafahamu haja kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Messi anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha kwanza cha Barcelona baada ya kufunga bao siku ya Jumamosi katika mechi ya ligi kuu ya La Liga.

Bayern, ambayo tayari imeshinda kombe la ligi kuu ya Premier ya Bundesliga, iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wake wa kutegemewa wakati wa mechi yao siku ya Jumamosi ambayo waliishinda Freiburg kwa bao moja kwa bila katika uwanja wa Allianz Arena.

Image caption Lionel Messi

Kocha Heynckes, anatarajiwa kuwajumuishwa wachezaji wake wote mashuhuri kwa mechi hiyo itakayochezwa nchini Uhispania, lakini Nahodha Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger, Javi Martinez, Luiz Gustavo, Dante naMario Gomez wote watalazimika kucheza kwa umakini ili kuzuia kadi nyingine ya njano.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi, ambaye amefunga magoli 54 baada ya kucheza mechi 45 msimu huu, amerejelea hali ya nzuri baada ya kuuguza jeraha la paha katika siku za hivi karibuni.

Katika mechi ya ligi kuu ya La Liga, alicheza dakika 32 wakati wa mechi yao na Athletic Bilbao ambayo walitoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili.