Deco taabani dawa za kuongeza nguvu

Deco
Image caption Deco aliyekuwa mchezaji wa Chelsea

Aliyekuwa mcheza kiungo wa Chelsea na wa timu ya taifa ya Ureno Deco amepatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli iliyoharamishwa ya diuretic furosemide, nchini Brazil.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, alipatikana na hatia hiyo kufuati ushindi wa klabu ya Fluminense dhidi ya Boavista tarehe 30.

Dawa hiyo iliyopigwa marufuku ina uwezo wa kuficha dawa zingine za kusisimua misuli.

Hata hivyo mawakili wa mchezaji huyo wamesema tatizo hilo lilisababishwa na vitamini zilizoharibika.

Klabu ya Fluminense imesema haiwezi kusema lolote hadi matokeo ya uchunguzi zaidi yatakapotolewa siku ya Ijumaa.

Mchezaji huyo wa Ureno mzaliwa na Brazil, aliichezea Chelsea kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka wa 2008 hadi 2010 na kucheza zaidi ya mechi 50.

Alishinda kombe la ligi kuu ya premier katika mwaka wake wa pili na Klabu ya Chelsea pamoja na mataji mawili ya kombe la FA mwaka wa 2009 na 2010.

Deco ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wamewahi kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya akiwa na vilabu viwili tofauti Barcelona mwaka wa 2006 na FC Porto mwaka wa 2004.