Ferguson kufanyiwa upasuaji

Image caption Sir Alex Ferguson

Kocha wa Manchester United amesema hana mipango ya kustaafu hata baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa kocha huyo atafanyiwa upasuaji baadaye mwaka huu.

Ferguson, 71, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kiuno Baada ya kukamilika kwa msimu huu.

Ferguson anasema upasuaji huo hautaharibu mipango yake ya hapo baadaye na ana matumaini makubwa kuwa ataendelea na majukumu yake kama kawaida.

Nchini Uholansi, klabu ya Ajax inasherehekea ushindi wake wa tatu mfululizo wa ligi kuu ya premier, baada ya kuilaza Willem Tilburg kwa magoli matano kwa yai.

Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kuwa na alama nne zaidi kuliko wapinzani wao wa karibu PSV Eindhoven huku ikiwa imesalia mechi moja tu kabla ya kukamilika kwa ligi kuu ya premier nchini Uholansi.

Na klabu ya Juventus imeshinda kombe la ligi kuu ya serie A, ya Italia baada ya kuilaza Palemo kwa bao moja kwa bila hii leo.

Arturo Vidal aliifungia Juventua bao hilo muhimu na la ushindi kunako dakika ya hamsini na tisa kupitia mkwaju wa penalti na kuiweka juventus alama 14 mbele ya mahasimu wao wa karibu Napoli.