Oscar Pistorius hatashiriki mwaka 2013

Image caption Oscar Pistorius hayuko hali nzuri kiakili kushiriki mwaka 2013

Mshindi wa dhahabu wa mbio za walemavu Oscar Pistorius hatashiriki katika mashindani yeyote mwaka huu kwani anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya mauaji.

Pistorius, mwenye umri wa miaka 26, ambaye yuko nje kwa dhamana ameshitakiwa kwa kumuuwa mpenzi wake Bi Reeva Steenkamp, hajakatazwa na waandalizi kushiriki mbio zozote.

Wakala wake , Peet van Zyl, amesema mshindi huyo wa mbio za walevamu za Olimpiki mara sita hali yake ya kiakili kwa wakati huu bado haimruhusu kushiriki katika amshindano yeyote.

"Mimi na hata kocha wake(Ampie Louw) hatujawahi kumshinikaza aanza kushiriki mashindanoni, ni uamuzi wake yeye mweyewe," amesema Van Zyl.

Pistorius alikamatwa tarehe 14 Februari mwaka huu baada ya kumpiga risasi na kumuua Bi Steenkamp na tangu wakati huo haja shiriki katrika mashindano yeyote.

Mwanariadha huyo amekanusha kosa la mauaji na anadai kwamba alimpiga mpenzi wake risasi kimakosa kwani alifikiria ni jambazi aliyekuwa amevunja nyumba yake.

Tarehe 22 Februari Pistorius aliachiliwa kwa dhamana na kuondolewa vikwazo ambavyo vingelimzuia kushiriki katika mashindano ya riadha.