Paolo Di Canio kutimua wachezaji

Image caption Kocha Paolo Di Canio aonya wachezaji

Meneja wa Sunderland Paolo Di Canio ametishia kuwafukuza wachezaji ambao wamekiuka maadili ya klabu.

Wachezaji wawili Phil Bardsley and Matthew Kilgallon,ambao walipigwa picha wakiwa katika jumba la kuchezea kamare hawakujumuishwa katika kikosi kilicho fungwa 1-0 na Tottenham siku ya Jumapili.

Hivi majuzi Di Canio aliwapiga faini wachezaji saba kwa utovu wa nidhamu akisema tabia nyengine zinasikitisha sana.

"Hawa wachezaji hawatakuwa hapa mwaka ujao - sio chini yangu", alinukuliwa akisema bila kutaja ni wachezaji gani aliokuwa akiwazungumzia.

Amesema: " mwenye Klabu pamoja na mimi tutakaa tujadiliane lakini tayari anafahamu mambo mengi".

Di Canio pia alifichua kuwa kuna mchezaji wake mmoja ambaye hakuja mazoezini kwa kisingizio ya matatizo ya tumbo kutokana na kula chakula kibaya hata hivyo mchezaji huyo alizima simu yake na daktari wa timu hakuweza kuwasiliana naye.

Bao lililofungwa na Gareth Bale katika dakika ya 90 iliipa ushindi Tottenham hivyo kuiacha Sunderland katika nafasi ya 17 ya ligi kuu ya Uingereza .