Cole kuihama West Ham

Image caption Carlton Cole

Mshambuliaji wa West Ham Carlton Cole, amesema ataihama klabu hiyo msimu ujao, baada ya wasimamizi wa klabu hiyo kuamua kutompa kandarasi mpya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na na tisa ameichezea West Ham kwa muda wa miaka saba iliyopita, lakini hajakuwa katika hali nzuri msimu huu na amefunga magoli mawili pekee.

Nafasi ya mchezaji huyo haijulikani hasa baada ya West Ham kumsajili Andy Carol na kuumpa mkataba wa kudumu.

Kocha wa West Ham Sam Allardyce, amesema Carlton anastahili kuwa katika hali nzuri kwa sasa ukizingatia umri wake na kwa kuwa hatuna nafasi kwa sasa tumeona ni vyema kuumpa nafasi atafute klabu nyingine itakayompa hiyo nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Cole, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mara saba alijiunga na West Ham mwaka wa 2006 kutoka klabu ya Chelsea.

Alifunga goli lake la mwisho na West Ham, Desemba mwaka uliopita wakati waliposhindwa na Everton katika uwanja wao wa nyumbani wa Upton Park.