Nani atakuwa bingwa Bayern au Dortmund?

Image caption Jurgen Klopp

Kocha wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp anaamini kuwa fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, katika uwanja wa Wembley, itakuwa ya kusisimua na ya Kihistoria.

Fainali hiyo ambayo ni ya kwanza kwa timu za Ujerumani kukutana.

Klabu ya Klopp itachuana na mabingwa wa ligi kuu ya Bundesliga Bayern Munich kuanzia saa nne kasorobo za usiku, majira ya Afrika Mashariki.

Mcheza kiungo wa Dortmund Mario Gotze, atakosa fainali hiyo kutokana na jeraha la mguu na anatarajiwa kujiunga na Bayern baadaye mwaka huu

Mchezaji wa kimataifa wa Japan Shinji Kagawa, alikihama klabu hiyo ya Dortmund na kujiunga na Manchester United juni mwaka wa 2012, kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili naye Gotze atasajiliwa na Bayern kwa kitita cha pauni milioni thelathini na moja nukta tano.

Klopp, mwenye umri wa miaka 45, amesema ufuasi wa katika mchezo wa soka nchini Ujerumani, umegeuka na kuwa kama dini.

Mwaka wa 2005, miaka minane baada ya kushinda kombe hilo la klabu bingwa barani Ulaya Dortmund, nusura itangazwe kuwa imefilisika, hali ambayo Klopp anafahamu wazi kuwa haiwezi kuruhusiwa kutokea tena.

Tangu mwaka huo klabu hiyo imechukua maamuzi ambayo yameifanya klabu hiyo kuandikisha matokeo mema na pia kuimarisha mapato yao, baada ya kuwavutia mashambiki wengi na wadhamini.