Bayern Munich Mabingwa wapya wa Ulaya

Image caption Bayern Munich

Arjen Robben aliifungia klabju yake ya Bayern Munich goli dakika za mwisho mwisho za mechi yao ya fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund, na kuisadia mabingwa hao wa ligi ya Bundesliga ya Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Ushindi huo kwa Bayern wa magoli mawili kwa moja sasa unafuta rekodi yao mbaya ya kupoteza kombe hilo mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikiwemo, kushindwa kwao na Chelsea mwaka uliopita katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena, kupitia mikwaju ya penalty.

hata hivyo Bayern sasa wameandikkisha historia nyingine ya kushinda kombe hilo kwa mara ya tano katika historia ya klabu hiyo.

Vilabu vya Real Madrid na Ac Millan ndivyo vimewahi kushinda kombe hili mara nyingine zaidi.

Real Madrid imeshinda mara tisa nayo Ac Millan imeshinda mara saba.

Kocha wa Bayern Jupp Heynkes ambaye anakamilisha kandarasi yake na Bayern sasa anaiga klabu hiyo kwa furaha baada ya kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Pep Gaurdiola anatarajiwa kuchukua mahala pa Heynkes msimu ujao.