Michuano ya kufuzu kombe la dunia yapamba moto

Wachezaji wa Ivory Coast
Image caption Wachezaji wa Ivory Coast

Michuano ya kufuzu kwa kombe dunia kanda ya afrika imeendelea mwishoni mwa juma hili huku kukiwa na mechi kadhaa.

Ivory Coast na Ethiopia ziliandikisha rekodi ya kuwa timu za kwanza kufuzu kwa hatua ya muondoano.

Ivory coast imeilanza Tanzania magoli manne kwa mawili katika mechi ya kundi C mjini Dar.kufuatia ushindi huo ivory coast imejikatia tikiti ya raundi ya mwisho huku ikiwa imesalia na mechi moja.

Misri vile vile imefuzu katika kundi D chini ya kocha wao mpya Mmarekani Bob Bradley.

Mjini Addis Ababa wenyeji Ethiopia waliilaza Bafana Bafana ya Afrika Kusini kwa magoli mawili kwa moja na hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia itakayoandaliwa nchini Brazil mwaka ujao.

Kebede aliifungia ethiopia bao la kwanza kunako dakika ya 42, kabla ya mchezaji wa Afrika Kusini, Parker kujifunga mwenyewe.

Afrika Kusini ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa mechaji huyo hjuyo aliyejiunga scot Parker dakika ya 34.

Katika kundi cha Tanzania, walinyukwa magoli manne kwa mawili katika mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar.

Image caption Wachezaji wa Misri

Taifa stars ilipata magoli yake kupitia kwa Amri Kiemba na Tom Ulimwengu maarufu kama grader.

Ivory coast kwa upande wake ilipata magoli yake kupiti kwa Traore kadika ya kumi na tatu, Kalou Toure dakika 23 na dakika ya 44 kwa njia ya penalti kabla ya Bony kufunga la mwisho dakika ya 90.

Gambia nayo ilinyeshwa magoli mawili bila jibu na Morocco.

Katika kundi D, Ghana imeimarisha matumaini yake ya kufuzu baada ya kuilaza lesotho kwa m agoli mawili kwa yao.

Ghana sasa ina alama 12 ikifuatwa na zambia na alama 11.

Sudan na Lesotho tayari zimebanduliwa nje ya mashindano hayo.

Misri imefuzu katika kundi G baada ya kuilaza Mozambique kwa bao moja kwa bila.