Kenya yapata dhahabu ya kwanza Moscow

Image caption Edna Kiplagat akimaliza mbio mjini Moscow

Mashindano ya mbio za dunia yameanza hii leo mjini Moscow Urusi.

Bingwa mtetezi wa mbio za marathoni kwa upande wa wanawake Edna Kiplagat kutoka Kenya ametetea taji lake mapema jumamosi asubuhi baada ya kushinda medali ya dhahabu.

Kiplagat ameshinda mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 25 na sekunde 44.

Valeria Straneo wa Italia ameshika nafasi ya pili licha ya kuongoza kwa muda mrefu kwenye mbio hizo, lakini Kiplagat alianza kumuacha walipofika kilometa 40 na kumaliza mbio kwa zaidi ya sekunde 15 nyuma ya Straneo.

Kayoko Fukushi wa Japan ameshika nafasi ya tatu na kuchukua medali ya shaba.

Hii ni medali ya kwanza ya Kenya ya dhahabu kwenye mashindano hayo ya dunia yanayoandaliwa na shirikisho la riadha duniani IAAF.