Jamaica yanyakua relay. Mbio za mwisho.

Image caption Usain Bolt wa Jamaica

Usain Bolt ameongoza Jamaica kupata ushindi katika mbio za kupokezana mjini Moscow.

Bolt anafikisha idadi kamili ya medali zake za dhahabu kufikia 8.

Bolt aliongoza timu yake kupata ushindi wa sekunde 37.36 huku Marekani ikichukua nafasi ya pili na Uingereza kupata, awali , nafasi ya tatu.

Hata hivyo Uingereza ilipokonywa medali yao ya shaba baada ya malalamiko kuwa walivunja kanuni za mbio hizo wakati wa kubadilishana kwa mkimbiaji wa pili, aliyevuka msitari wake kwa hiyo Canada ikapandishwa kwa nafasi ya tatu.

Bolt amemaliza mashindano hayo akiwa na medali tatu za binafsi za dhahabu baada ya kunyakua mbio za mita 100, 200 na hizo za kupokezana.

Amewafikia wamarekani Michael Johnson, Allyson Felix na Carl Lewis ambao wote wana medali za dunia nane kila mmoja.