Manchester City yainyuka Newcastle

Goli la pili la Manchester City
Image caption Goli la pili la Manchester City

Meneja mpya wa Manchester City Pellegrini amefurahia ushindi wake wa kwanza katika ligi ya England kwa kuifunga NewCastle 4-0.

David Silva amekuwa wa kwanza kuliona lango kunako dakika ya 6 tu ya mchezo kabla ya Sergio Aguero kupachika bao la pili kwenye dakika ya 22.

Newcastle ilionekana kushindwa kumudu gonga za hapa na pale za wachezaji wa City hadi mchezaji wao Taylor kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mambo yamezidi kuwa mabaya kwa wageni na kunako dakika ya 51 mkwaju wa mita 20 kutoka kwa Yaya Toure ukaishia langoni likawa bao la tatu.Samir Nasri imefunga kazi kwenye dakika ya 75 kwa kuingiza goli la 4.

Manchester City katika mechi hiyo ya kwanza imeonekana kuwa na kikosi kilichokamilika na chenye mchezo wa kuvutia zaidi.

Ilitumia pesa nyingi kuingiza damu mpya katika kikosi chake kwa kuwanunua Fernandinho,Jesus Navas na Alvaro Negredo.