Manchester City yainyuka Hull 2-0

Yaya Toure na Samir Nasri
Image caption Wachezaji wa Man City wakisherehekea

Manchester City imeishinda Hull City uwanjani Etihad ,lakini licha ya ushindi huo kiwango chake hakijaridhisha.

Alvaro Negredo kutoka benchi amenusa nyavu kwa goli aliloingiza kwa kichwa baada ya saa nzima ya mchezo kabla ya Yaya Toure kufunga bao la pili kwa mkwaju wa free-kick aliopiga kwa ustadi mkubwa.

Hull iliweza kupata nafasi kubwa za kufunga bao katika kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji Sone Aluko alishindwa kumalizia katika lango lililokuwa limeachwa wazi na kipa Joe Hart.

Manchester City ilionekana bado kutetereka katika safu yao ya ulinzi baada ya kukosa tena huduma za mlinzi Vicent Kompany ambaye bado anauguza jeraha.