Arsenal waidunga Tottenham

Image caption Arsenal waifunga Tottenham

Arsenal waendeleza rekodi yao ya kutofungwa na Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani baada ya kuwazaba vijana wa Andre Villas-Boas bao moja kwa sufuri.

Tangu mwaka wa 1993 Tottenham imewahi kuifunga Arsenal nyumbani mara moja tu.

Kwa kocha huyo mreno ni siku ya masikitiko kwani ndio mechi yake ya kwanza kwa timu yake kupoteza tangu msimu huu uanze.

Ilikuwa ni katika dakika ya 23 wakati Olivier Giroud alipofunga baada ya kupewa pasi na Theo Walcott .

Katika dakika za lala salama za kipindi cha pili licha ya Tottenham kujenga hema katika ngome ya Arsenal lakini kipa Wojciech Szczesny alifanya kazi ya ziada kwa kuokoa mkwaju wa Jermain Defoe hivyo kuwanyima vijana wa Villas-Boas nafasi ya kulikomboa bao hilo.

Ushindi huu unamaanzisha kuwa vijana wa Arsene Wenger wamepanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi hiyo ya Uingereza.

Orodha ya Wachezaji

Arsenal 01 Szczesny 04 Mertesacker 06 Koscielny 25 Jenkinson 28 Gibbs 07 Rosicky Booked (Monreal - 79' ) 10 Wilshere (Flamini - 43' Booked ) 14 Walcott (Sagna - 90' ) 16 Ramsey 19 Cazorla 12 Giroud

Wachezaji wa akiba

21 Fabianski 03 Sagna 17 Monreal 20 Flamini 44 Gnabry 58 Gedion Zelalem 22 Sanogo

Tottenham Hotspur 25 Lloris 02 Walker 03 Rose 05 Vertonghen 20 Dawson 08 Paulinho 15 Capoue (Sandro - 75' ) 17 Townsend (Lamela - 75' ) 19 Dembele (Defoe - 69' Booked ) 21 Chadli 09 Soldado Booked

Wachezaji wa akiba 24 Friedel 16 Naughton 14 Holtby 22 Sigurdsson 30 Sandro 33 Lamela 18 Defo