Man United watoteshwa na Liverool

Image caption Liverpool waichapa Manchester United

Liverpool imejiweka katika nafasi nzuri sana kwenye ligi ya Uingereza baada ya kuwazima mabingwa wa ligi hiyo Manchester United kwa bao moja kwa bila katika uwanja wa Anfield.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Liverpool kuwa katika nasafi kama hii mwanzo mwanzo wa ligi tangu mwaka 1995.

Pia Liverpool inakuwa timu ya kwanza tangu mwaka 2011 kucheza mechi tatu mfululizo katika ligi hiyo bila ya kufungwa goli lolote.

Ilikuwa fursa nzuri kwa kuhitimisha miaka 24 tangu kuzaliwa kwa kuipatia Liverpool bao hilo la pekee na la ushindi.

Mwamba huyo alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa kwani alifunga kwa kichwa safi ambapo kipa wa Man U De Gea alishtukia wavu ukitikisika.

Ni mara ya tatu mfululizo kwa Sturridge kuivungia timu yake tangu ligi hii ya Uingereza ianze.

Image caption Daniel Sturridge mfunganji wa Liverpool

Kushindwa kwa Manchester United inachafua rekodi ya kocha wao mpya David Moyes kwani hata akiwa mkufunzi wa Everton hajawahi kuingozi timu yake kuifunga Liverpool katika uwanja wa Anfield.

Hata Robin van Persie alikuwa na siku mbaya kwani alikuwa na wakati mgumu kumfunga kipa mpya wa Liverpool Simon Mignolet, ambaye alizima ndoto ya Man U ya kupata bao.

Tangu mlinda lango huyo Mignolet, kuhamia Anfield kutoka Sunderland kwa kima cha £9m hajafungwa bao hata moja.

Orodha ya wachezaji

Liverpool 22 Mignolet 02 Johnson (Wisdom - 79' ) 03 Jose Enrique 05 Agger 37 Skrtel 08 Gerrard 09 Aspas Booked (Sterling - 60' ) 10 Coutinho (Alberto - 84' ) 14 Henderson 21 Lucas Booked 15 Sturridge

Wachezaji wa akiba

01 Jones 34 Kelly 38 Flanagan 47 Wisdom 06 Alberto 31 Sterling 33 Ibe

Manchester United 01 De Gea 03 Evra 04 Jones (Valencia - 37' ) 05 Ferdinand 15 Vidic 11 Giggs (Hernandez - 73' ) 16 Carrick Booked 18 Young Booked (Nani - 63' ) 19 Welbeck 23 Cleverley Booked 20 Van Persie Booked

Wachezaji wa akiba

13 Lindegaard 12 Smalling 28 Buttner 08 Anderson 17 Nani 25 Valencia 14 Hernandez