IOC wasubiri medali kutoka kwa Armstrong

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inamsubiri mwendesha baiskeli wa Marekani aliyepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini Lance Armstrong arejeshe medali shaba aliyoshinda kwenye mashindano ya Olimpiki ya mjini Sydney mwaka 200, kwa mujibu wa mkuu wa tume ya sheria ya IOC.

Kamati hiyo ya IOC ilimuandikia Armstrong mnamo mwezi Januari mwaka huu kumtaka arejeshe medali hio ingawa Bach alikiri kwamba mwendesha baiskeli huyo alikiri makosa yake lililobaki ni kutimiza ahadi yake ya kukabidhi medali.

Bach ameongezea kusema kua walitangaza matokeo hayo kua yasiyo sihi na nafasi hio kumkabidhi Abraham Olano wa Uhispania aliyemaliza wa nne.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ilichelewesha kumuadhibu Lance Armstrong hadi shirika linalotawala mchezo wa mashindano ya baiskeli (international Cycling Union -UCI) lilipoidhinisha hatua ya Armstrong kuchukuliwa hatua kufuatia majuma matatu ambapo mtuhumiwa alikua na fursa ya kukata rufaa.

Kilichofuata ni hatua ya kumnyanganya Armstrong medali zote saba alizoshinda kwenye mashindano ya mbio za Ufaransa maarufu kama Tour de France na kupigwa marufuku daima asishiriki mashindano mengine maishani mwake. Haya yalifuatia ushahidi wa shirika la Marekani linalopambana na matumizi ya dawa za kuongezea nguvu mwilini (USADA)

Baada ya ubishi mkali marafiki wa Armstrong walitoa ushahidi uliombana yeye na baadhi ya washirika wake kua kweli alitumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.