Roy Hodgson atetea England

Image caption England ilienda sare tasa na Ukrain matokeo ambayo yamewakera wengi

Meneja wa timu ya Uingereza Roy Hodgson, amesema aliridhika na walivyocheza wachezaji wake walipojitosa katika michuano ya kuwania kombe la dunia.

England ilienda ilimaliza mchezo kwa sare tasa dhidi ya Ukraine kwenye mechi iliyochezwa mjini Kiev

Kikosi cha Hodgson kinasalia juu katika kikundi cha H na kitafuzu ikiwa kitashinda mechi zao mbili za kufuzu dhidi ya Montenegro na Poland zitakazochezwa katiika uwanja wa Wembley.

Baadhi ya mechi ambayo walisema ilikosa msisimuko na ambayo ilichezwa mbela ya mashabiki 70,000, meneja huyo wa England alisema, "kabla ya mchezo, hisia waliyokuwa nayo wengi ni kwamba matokeo ya sare yoyote hayatakuwa mabaya.''

England iliingia kwenye mchezo huo, bila ya wachezaji, Danny Welbeck ambaye huchezea Man U , Wayne Rooney na mshambulizi wa Liverpool Daniel Sturridge ambao hawakucheza kutokana na majeraha.

Uwezo wetu wa kushambulia ulikuwa mdogo sana kwa sababu hatukuwa na wachezaji, Rooney, Welbeck na Sturridge, alisema Hodgson.

"pia tulimpoteza kiungo cha kati, Alex Oxlade-Chamberlain kwa sababu ya jeraha la goti ingawa wachezaji waliowakilisha kwenye mchezo huo walicheza vyema.

Sare hiyo iliisongesha England mbele kwa pointi moja kwenye kundi la H ikisalia na michuano miwili.