Arsenal yatembeza kichapo

Arsenal watamba
Image caption Arsenal watamba

Aaron Ramsey alishinda magoli 2 na kuiwezesha timu yake kuinyoa Sunderland 3-1 huku meneja Paolo Di Canio akipewa kadi nyekundu.

Goli la kwanza lilipatikana baada ya kuhudi za mchezaji mpya aliyesajiliwa na Arsenal Mesut Ozil ambaye alimwandalia pasi murua Olivier Giroud aliyenusa nyavu. Goli hilo lakini lilisawazishwa na Craig Gardner muda mfupi baada ya mapumziko.

Magoli mengine mawili ya Arsenal yalitiwa kimiani na Ramsey na kuiwezesha timu yake kuandikisha ushindi wa mabao 3-1 ambao ni wa tano mfululizo.

Manchester City yapoteza mwelekeo.

katika mechi nyingine,Stoke City itajilaumu yenyewe kwa kupoteza nafasi kadhaa murua za kuishinda Manchester City katika mechi ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0

Manchester City ilitawala kipindi cha kwanza kwa kumiliki mpira lakini mara kwa mara wakashindwa kuvunja ngome ya Stoke ambao bado wanaendelea kufanya vyema katika tangu ligi ilipoanza.

Matokeo haya hayamsaidii lolote meneja mpya wa Manchester City kwa kuwa bado anahangaika kuisuka timu hiyo na haijacheza kwa kiwango chake.