Chelsea yakabwa koo na Everton

Wachezaji wa Chelsea
Image caption Wachezaji wa Chelsea

Goli la kichwa lililofungwa na mchezaji mpya wa Everton Steven Naismith limemkaribisha Jose Mourinho katika ligi ya premier.

Hicho ni kipigo cha kwanza alichokipata meneja wa Chelsea Jose Mourinho tangu kurudia kwake katika ligi ya England kuifundisha Chelsea.

Steven Naismith amefunga goli hilo kunako dakika ya 45 ya mchezo sekunde chache kabla ya timu zote kuingia katika mapumziko.

Chelsea ambayo imemuorodhesha mshambuliaji wake mpya Samuel Eto'o imefanya kila mbinu ili kugeuza matokeo hayo bila mafanikio.

Kabla ya mechi hiyo,Tottenham iliinyuka Norwich 2-0;Newcastle ikapata ushindi murua ugenini wa mabao 2-1 ya Aston Villa,Hull na Cardiff zikatoka sare 1-1,vile vile Fulham nayo ikatoka sare 1-1 na West Brom.

Arsenal,Tottenham na Liverpool zinaongoza zikiwa na alama 9 kabla ya mchuano wa Liverpool jumatatu itakaposafiri kwenye uwanja wa Swansea.