Ruud wa Uholanzi kocha mpya wa Tunisia

Image caption Kocha Ruud atakuwa nahodha wa Tunisia kwa kipindi cha miezi miwili

Aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Uholanzi, Ruud Krol ametia saini mkataba wa miezi miwili kuwa kocha wa timu ya Tunisia katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia barani Afrika.

Carthage Eagles watacheza na Cameroon kwa ligi mbili mwezi Octoba na Novemba ambapo mshindi atapata nafasi ya kucheza katika fainali za mwaka ujao nchini Brazil.

Krol pia atasalia kuwa kocha wa timu ya CS Sfaxien ,klabu ambayo alisimamia katika michuano ya Tunisia mwezi Mei.

Sfaxien pia wamefuzu kishiriki nusu fainali ya kombe la shirikisho.

Shirikisho la soka la Tunisia limemchagua Krol kuchukua nafasi ya Nabil Maaloul ambaye alijiuzulu baada ya timu hiyo kupoteza mechi ya finali ya makundi kwa mabao 2-0 didhi ya Cape Verde tarehe 7 Septemba.

Wakati huo huo matokeo hayo yalimaanisha kuwa Tunisia haikufuzu kushiriki katika fainali za makundi lakini baadaye walipata afueni wakati ilipobainika kuwa Cape Verde walishirikisha mchezaji asiyestahili wakati wa mechi hiyo.

Haya yalifuatiwa na shirikisho la soka duniani kutuza Tunisia ushindi wa mabao 3-0,na kuwaruhusu kuendelea katika fainali ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia barani Afrika