Man City yanyolewa na Aston Villa

Yaya Toure wa Man City
Image caption Yaya Toure wa Man City

Manchester City wamekosa nafasi ya kuwa miongoni mwa viongozi wa ligi waliposhindwa na Aston Villa 3-2.

Goli la kwanza lilifungwa na City kupitia nyota wao Yaya Toure ambaye ametoa matumaini kwa City ya kuondoka na ushindi wa kwanza wa ugenini.

Goli hilo lakini halikukaa kwa muda mrefu kabla ya kukombolewa Karim El Ahmadi.

Edin Dzeko alifufua matumani ya City kwa kufunga bao la pili.Lakini nalo likasawazishwa na Leandro Bacuna kabla ya Andreas Weimann kufunga kazi kwa kufunga bao la 3.

Katika matokeo mengine ni kwamba Cardiff imepata ushindi ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham,Hull ikainyuka West Ham goli 1-0 na Southampton kuibamiza Crystal Palace mabao 2-0.