Kipsang avunja rekodi ya Berlin Marathon

Wilson Kipsang
Image caption Kipsang katika

Mkenya Wilson Kipsang amevunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon kwa kupunguza sekunde 15 aliposhinda mbio za Berlin mapema jumapili.

Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliandikisha mda wa saa mbili dakika tatu na sekunde 23 kuondoa rekodi ya zamani iliyowekwa na Mkenya mwenzake Patrick Makau miaka miwili iliyopita.

Rekodi hiyo iliwekwa katika mji mkuu wa Ujerumani ambako Makau alikimbia kwa mda wa saa 2:dakika 03:na sekunde 38.

Wakenya wengine walioshiriki mbio a Berlin Eliud Kipchoge alimaliza katika mda wa saa 2:04:05) huku Geoffrey Kipsang akiweka mda wa saa 2:06:26 katika nafasi ya tatu.

Makau hakushiriki mbio hizi baada ya kujiondoa wiki mbili zilizopita kutokana na kuuguza jeraha la goti.

Wilson alifanya mazowezi akiwa na nia ya kuvunja rekodi ya Berlin na moja kwa moja alianza mbio za leo kwa kudhibiri uongozi katika hatua ya kilomita 10 za mwisho, akiwaacha wenzake walioonekana kuishiwa na pumzi ya kumkimbiza.

Baada ya mbio hizi Kipsanga alisema," Nimefurahi sana kwa ushindi huu na kwa kuvunja rekodi,"

"nilivutiwa mno na Paul Tergat wakati akikimbia na kuvunja rekodi hii miaka kumi iliyopita katika mashindano haya haya.

Ushindi wa Kipsang unampa jumla ya ushindi wa saba tangu aanze kushiriki mashindano ya marathon mjini Paris,Ufaransa miaka mitatu iliyopita.

Itakumbukwa kuwa Kipsang alishinda mbio za marathon za London mwaka jana na kwenye michezo ya Olimpiki alimaliza wa tatu na kujishindia medali ya fedha mjini London.

Ushindi wa mbio hizi za Berlin ni wa kwanza mwaka huu. Licha ya mbio za London kua mojapo ya mbio muhimu duniani na kwake aliweza kumaliza wa tano mapema mwezi Aprili mwaka huu.