Ferguson asema hatarudi ulingoni.

Image caption Ferguson asema katu hatakuwa kocha tena

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasisitiza kwamba hatazingatia kurejea katika shughuli za ukocha wa kandanda.

Manchester United hivi sasa wanashikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya England chini ya uongozi wa David Moyes, aliyeshikilia nafasi hiyo baada ya Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita.

"Mimi sina hamu ya kuwa meneja tena ,na kujisumbua roho yangu ," alisema Ferguson. "United wako mikononi mwa uongozi mzuri. David atakua poa. Ni meneja mzuri."

Ferguson, mwenye umri wa miaka 71,alidokeza kwamba Roman Abramovich alimtaka aiongoze Chelsea alipoinunua mnamo mwaka 2003.

"walimtuma wakala aniulize Abramovich alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza ya klabu hiyo lakini niliwaambia 'Ng'oo."