Mourinho akerwa na mswali

Image caption Morinho atakiwa kuondoka uwanjani na refa

Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho alikatiza mkutano na waaandishi habari baada ya kukerwa na maswali kumhusu Kevin de Bruyne.

Alisema Juan Mata, ambae hivi karibuni hakuhusishwa sana na mechi za Chelsea atakua katika timu itakayopambana na Steaua Bucharest katika mchuano wa Jumaanne wa kombe la klabu bingwa ya Ulaya lakini De Bruyne ameachwa nyumbani baada ya kutocheza vizuri msimu huu.

"kwa majuma matatu mmekua mkiongea kuhusu Mata, na sasa zamu ya De Bruyne," alisema.

"kwa hiyo mnashughulishwa na wasiocheza badala ya wanaocheza?"

Baada ya kuhojiwa kuhusu kutocheza kwa Mata katika wiki za hivi karibuni Mourinho alionekana kutofurahishwa na maswali kuhusu sababu za kutomchezesha Mbelgiji huyo na akakatiza papo hapo mkutano wake na waandishi habari nchini Rumania.

Mata anaechezea timu ya taifa ya Hispania na mchezaji bora wa Chelsea katika msimu uliopita amecheza mechi mbili tu kati ya sita za ligi ya Premier msimu huu.

De Bruyne, ambae aliichezea Chelsea katika mchuano wa kombe la Capital One Cupambapo waliishinda Swindon 2-0 wiki iliyopita lakini hakuchaguliwa katika kikosi kilicjhotoka sare 1-1 dhidi ya watani wao Tottenham mnamo siku ya Jumaamosi.

Mourinho aliongeza kusema "De Bruyne hakuteuliwa. Ni uamuzi wangu.11 tu wanaweza kucheza na 18 wanaweza kuteuliwa.Mimi huamua kutokana na jinsi wanavyotenda uwanjani wanapocheza ama wanapokua mazoezini.Lakini tabia yenu ni kuuliza tu kuhusu wachezaji wasioteuliwa katika timu. Na tuonane Jumaanne."