Sebastien Vettel aonyesha umahiri

Vettel
Image caption Sebastien Vettel

Timu ya magari ya Red Bull pamoja na dereva wake Sebastian Vettel wametoa mfano unaofaa kuigwa wa mchezo wa mbio za magari kwa ustaadi wa dereva huyo na ubora wa gari kwenye mbio za Korea jumapili.

Huu ukiwa ushindi wa mara nne mfululizo na wa nane msimu huu na mara 34 katika kipindi kifupi cha kushiriki mashindano.

Mpinzani wake wa karibu Fernando Alonso wa timu ya magari ya Ferrari aliweza tu kumaliza katika nafasi ya sita na hivyo kumfungulia Mjerumani fursa ya kutangazwa mshindi wa mashindano haya msimu huu wa 2013 kwenye mashindano yatakayofanyika nchini Japanjumapili ijayo.

Na kwenye mashindano ya mchezo wa Tennis ya Uchina au China open aliyekua mchezaji bora duniani Novak Djokovic alionyesha sababu ya kushikilia hadhi hio kwa mda mrefu kwa kumkandika mtani wake Rafael Nadal 6 -3, 6 -4 na hivyo kutoa ushindi wa Kombe la China.

Hata hivyo licha ya kushindwa Rafael Nadal atatangazwa mchezaji bora duniani bora kwa kuweza kufika fainali ya China.