Arsenal yazidi kutamba

Arsenal wakishangilia ushindi
Image caption Arsenal wakishangilia ushindi

Ushindi wa Arsenal dhidi ya Norwich umeiwezesha kwendelea kuongoza ligi kuu ya premier ya England.

Mesut Ozil amefunga mabao 2 miongoni mwa 4-1 yaliyofungwa na Arsenal kwenye uwanja wao wa Emerates.

Goli la kwanza limefungwa na Jack Wilshere kwa ustadi mkubwa kunako dakika ya 17 ya mchezo.Mesut Ozil amepiga la pili kunako dakika ya 57 kabla ya Norwich kupata bao lao lililoingizwa na Jonathan Howson dakika 10 baadae.

Aaron Ramsey amepachika goli la 3 la Arsenal kwenye dakika ya 82 na Ozil kufunga kazi dakika 3 kabla ya kipenga cha mwisho kulia.

Kwa ushindi huo Arsenal inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 19 baada ya mechi 8 zilizokwisha chezwa.inafwatiwa na Chelsea yenye alama 17 sawa na Liverpool,lakini wanatofautiana kwa magoli.