Matokeo ya ligi kuu ya England

Olivier Giroud wa Arsenal
Image caption Olivier Giroud wa Arsenal

Arsenal bado inaongoza ligi kuu ya England kufuatia ushindi wao dhidi ya Crystal Palace.

Ushindi wa Arsenal umepatikana katika kipindi cha pili.Goli la kwanza limefungwa na Mikel Arteta kwa njia ya penalty kabla ya Olivier Djiroud kufunga kazi dakika chache kabla ya kipenga cha mwisho kulia.

Manchester United yaepuka kichapo.

Katika mechi nyingine zilizochezwa,Manchester United imetoka nyuma na kushinda mechi yake dhidi ya Stoke mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 katika kipindi cha kwanza.

Matokeo mengine Everton ikichezea ugenini imeifunga Aston Villa magoli 2-0.Norwich imetoka sare na Cardiff bila kufungana.Liverpool ikailima West Bromich mabao 4-1 yakiwemo 3 yaliyotiwa kimiani na Luis Suarez na Southampton ikaifunga Fulham

Kwenye msimamo wa muda wa ligi kuu ya England,Arsenal ni ya kwanza ikiwa na alama 22 ikifuatiwa na Livepool yenye alama 20.