Arsenal yaifumua Liverpool 2 - 0

Arsenal imeilaza Liverpool kwa jumla ya magoli 2 - 0 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates jijini London.

Arsenal walianza kuandika goli la kwa kwanza lilofungwa na Santiago Cazorla katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza baada ya kipa wa Liverpool Simon Mignolet kuutema mpira na kurudi uwanjani.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Arsenal walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa goli 1 - 0.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani na kuanza kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika ya 59 Aaron Ramsey alinogesha sherehe ya Arsenal kwa kupachika goli pili.

Kwa matokeo hayo Arsenal sasa itakuwa imejiimarisha kileleni mwa msimamo ligi kuu ya England kwa kujikusanyia jumla ya pointi 25.