Man United yaiadhibu Fulham 3 - 1

Manchester United imeiadhibu Fulham kwa jumla ya magoli 3 -1 katika mechi nyingine ya Ligi kuu ya England iliyochezwa siku ya jumamosi.

Goli la kwanza la Manchester United liliwekwa wavuni na Antonio Valencia katika dakika ya 9 baada ya mpira kuanzia kwa Robin van Persie ambaye alimpasia Wayne Rooneyaliyepelekwa mpira moja kwa moja kwa Valencia aliyeutumbukiza mpira moja kwa moja wavuni.

Karamu hiyo ya magoli iliendelea baada ya Robin van Persie katika dakika ya 20 kupachika goli la pili, ambapo pia dakika mbili tu baadae naye Wayne Rooney katika dakika ya 22 alipokea pasi kutoka kwa Robin van Persie na kuupachika mpira kimiani kirahisi.

Goli la kufuta machozi la wenyeji Fulham lilifungwa dakika ya 65 na mshambuliaji wa pembeni wa Fulham Alex Kacaniklic aliyeachia shuti kali ambalo Wayne Rooney alijaribu kuokoa bila mafanikio na kwenda moja kwa moja wavuni.