Spurs yadaiwa kutomjali goli kipa

Image caption Kocha wa Tottenham Andres Villas Boas

Klabu ya Tottenham imeelezwa kutojali afya kwa kumruhusu mlinda mlango wake Hugo Lloris kucheza mechi dhidi ya Everton baada ya kupoteza fahamu.

Lloris alipata jeraha kuchwani baada ya kuumizwa Romelu Lukaku wa Everton aliyemjeruhi na mguu wake katika mechi ya siku ya jumapili ambapo mpambano huo ulimalizika kwa kutoka suluhu ya kutokufungana.

Kocha wa Spurs Andre Villas- Boas ametetea uamuzi wa kumuacha Lloris kuendelea na mchezo.

Nafasi ya mlinda mlango huyo awali ilitazamaiwa kuchukuliwa na Brad Friedel.huku Lloris akitolewa nje ya uwanja lakini alionekana yu tayari kuendelea na mchezo hatua iliyomfanya Villas-Boas kutofanya mabadiliko yeyote.

Msemaji wa Taasisi ya afya ya Headway, Luke Griggs amesema mchezaji anapopata jeraha kichwani ni wazi anaweza kupoteza fahamu na ni muhimu wakapatiwa uangalizi wa karibu wa kitabibu.

Taasisi hiyo imesema kuwa mchezaji huyo kuendelea na mchezo kunaweza kusababisha madhara zaidi kwa mchezaji, hivyo alipaswa kuondolewa uwanjani mara tu baada ya kuumia na kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.