Pellegrini ajinadi kushinda

Image caption Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini

Kocha wa timu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema timu yake ina uwezo ya kuichapa timu yeyote iliyo miongoni mwa timu zilizosalia kwenye ligi ya mabingwa baada ya kufuzu katika hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza.

City ilifanikiwa kufuzu baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya CSKA Moscow.

Magoli matatu ya Alvaro Negredo na mawili ya Sergio Aguero yalitosha kuipa ushindi Man City.

Pellegrini amejisifu kuwa na timu yenye nguvu na kuwa walikuwa na malengo ya kufuzu kwenda raundi nyingine

Man City imefurahia hatua hii kwa kuwa ni mafanikio ambayo klabu hiyo haikuwahi kupata katika kipindi cha misimu miwili iliyopita.