Nani mwanasoka bora zaidi Afrika?

Image caption Fursa ni yako kumchangua mwanasoka unayedhani ni nyota zaidi barani Afrika kati ya hawa watano

Majina ya wanaowania taji la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka wa 2013 yametangazwa rasmi hii leo kupitia kipindi cha kiswahili cha Amka na BBC

Yaya Toure wa Ivory Coast yuko katika orodha hiyo kwa mara ya tano mtawalia ,wengine katika orodha hiyo ni Victor Moses na John Mikel Obi wa Nigeria, Jonathan Pitripia wa Bukina Faso na Pierre- Emerick Aubameyang wa Gabon.

Mshindi atateuliwa na mashabiki wa kandanda ambao wanapiga kura hadi tarehe 25 Novemba saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki. Ili kupiga kura kwenye mtandao tembelea wavuti huu: http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/african/

Unaweza kupiga kura kwenye tovuti hii ama kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia nambari ifuatayo +44 7786 20 20 08:

Tuma 1 ili kumpigia kura Pierre-Emerick Aubameyang

Tuma 2 ili kumpigia kura Victor Moses

Tuma 3 ili kumpigia kura John Mikel Obi

Tuma 4 ili kumpigia kura Jonathan Pitroipa

Tuma 5 ili kumpigia kura Yaya Toure

Gharama ya ujumbe ni kulingana na kanuni za kimataifa tafadhali thibitisha na mhudumu wako.Ni sharti utume ujumbe mmoja pekee kwa kila nambari ya simu.

Mshindi atatangazwa Jumatatu tarehe 2 Disemba saa Mbili na dakika thelathini na tano Usiku saa za Afrika Mashariki katika kipindi cha BBC cha (Focus on Africa) katika redio na runinga.

Hakuna mchezaji katika orodha ya mwaka huu aliyeteuliwa kutokana na kura za wanahabari 44 wa Afrika amewahi kushinda shindano hili la BBC.Wawili kati yao – Jonathan Pitroipa na Pierre- Emerick Aubameyang- ndio wa kwanza katika orodha hiyo kutoka mataifa yao.

Aubameyang, mwenye miaka 24,amekuwa mchezaji mzuri sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita-na kumaliza msimu wa mwaka 2012-2013 akiwa ameingizia klabu yake St-Etiennemabao 19, na kumweka wa pli,kwenye orodha ya wachezaji bora zaidi kwenye ligi ya Ufaransa. Alisaidia klabu yake kushinda kombe lake la kwanza.

Mchezo wake ulimuwezesha kuhamia klabu ya Borussia Dortmund, na tayari ameingizia klabu hiyo ya Ujerumani mabao 11.

Mchezo wa Pitroipa ulianza kushika kasi alip[otajwa kuwa mcherzaji bora wakati wa michuano ya taifa bingwa Afrika iliyochezwa nchini Afrika Kusini ambapo pia alisaidia Burkina Faso kufika fainali ya michuano hiyo.

Pitroipa ameendelea kunga'aa na hata kuingizia nchi yake mabao matatu katika michuano ya kuwania nafasi ya kushiriki kwenye kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Wachezaji wawili walifanya hata vyema zaidi katika kombe la mataifa bingwa mwaka huu; ni pamoja na Mikel na Moses wote waliohusika pakubwa katika kufanikisha mchezo wa Nigeria hadi wakashinda kombe hilo mara ya kwanza katika miaka 19.

John Mikel Obi, mwenye umri wa miaka 26, pia alishinda kombe la Uropa akichezea Chelsea, wakati mwaka 2013 ndipo aliweza kuingizia Chelsea bao lake la kwanza baada ya kucheza mechi 185.

Mabao yamekuwa yakija kwa kasi kwa mchezaji VictorMoses mwenye umri wa miaka 22 huku akiingizia Chelsea mabao sita kabla ya kuhamia Liverpool, alikoingiza bao lake la kwanza mwezi Septemba.

Yote tisa, kumi ni kuwa mchezaji mwingine nyota ni Yaya Toure ambaye ni kiungo cha kati. Toure mwenye umri wa miaka 30, raia wa Ivory Coast, ameingiza mabao 12 hadi sasa mwaka huu pekee.

Ingawa yeye na wachezaji wenzake wa Man City, walipokonywa ushindi wa ligi ya Premier msimu uliopita, Toure bado alikuwa ngome imara uwanjani , huku akiwika sana mbele ya lango la bao.