Yaya Toure

Kwa wengi anajulikana na kukubalika kama mmoja wa Viungo bora katika kizazi cha sasa cha wanasoka.Yaya Toure ni roho ya Timu huku akitawala na kuheshimika pande zote.

Mwanasoka huyu alijiunga na Klabu yake ya sasa ya Manchester City mwaka 2010 na tangu wakati huo ameshinda Taji la Ubingwa wa Ligi kuu ya Kandanda England likiwa ni taji la kwanza kwa Timu hiyo katika miaka 44,vile vile Kombe la FA,na pia ngao ya Jamii kwa Mabingwa hao wanaovalia Jezi ya Blue ya mawingu.

Toure ambaye tayari ameishacheza zaidi ya mechi 109 kwenye klabu hiyo na kufunga magoli 23,yakiwemo magoli ya rekodi yatokanayo na Mipira ya adhabu,na ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika klabu hiyo.

Alijunga na Manchester City akitokea Barcelona ambako alikaa kwa miaka mitatu huku akitwaa mataji kadhaa ikiwa ni pamoja na Ubingwa wa Ligi kuu ya Spain mara mbili,Ubingwa wa Ulaya mara moja,Na Kombe la Super Cup na pia taji la klabu bingwa ya Dunia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 vile vile amekwishatwaa Ubingwa wa Soka huko Ugiriki akiwa na Klabu ya Olympiacos,na pia Ubingwa wa Ligi kuu katika nchi yake ya asili Ivory Coast.

Jambo la Kusikitisha kwa Yaya Toure ni katika medani ya kimataifa ambapo kizazi cha wanasoka kinachoaminika kuwa kizazi cha dhahabu katika soka la Ivory Coast kimeshindwa kutwaa Kombe ambalo limekuwa likitarajiwa kutoka kwao.Kwa kufungwa na Zambia mwaka 2012 katika Mechi ya Fainali ya Kombe la Mataifa yalikuwa matokeo yaliyoleta mshtuko katika Soka Barani Afrika.

Hata sasa akiwa na umri wa miaka 30 Yaya Tore bado hajaonyesha dalili za kushuka kiwango ambapo ameanza vema msimu huu wa soka akiwa na Klabu yake na Manchester City ambapo hadi sasa amekwishatia nyavuni bao 7.huku akiendelea kuonyesha kiwango cha juu cha Ubora.

Akiwa amekwishatwaa mara mbili taji la Mwanasoka bora wa mwaka wa Shirikisho la sokak barani Afrika CAF, Yaya Toure vile vile ni Mwanasoka pekee kutoka Barani Afrika kwenye orodha ya wachezaji 23 waliiorodheshwa kuwania tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA mwaka huu 2013.

WADADISI WASEMAJE KUMHUSU TOURE?

Ian Hughes ,ambaye ni Mwandishi wa Habari za Michezo wa BBC anasema kuwa msimu wa mwaka 2013 unaweza ukawa si mzuri kwa Yaya Toure kwa Upande wa Mataji,lakini bado Mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast,ameonyesha kasi, Nguvu,ubunifu,Magoli ya Kufunga,na hata Uongozi.

Viwango hivyo vya Ubora vimemtambulisha Yaya Toure kama mmoja wa Viungo waliokamilika pengine bora kabisa katika eneo la kati kati ya Dimba.Ni vigumu kufikiria zaidi yake anayetawala kwa sasa eneo hilo katika mchezo wa Kandanda unaopendwa na wengi.

Yeye ndiye mchezaji pekee kutoka Barani Afrika kwenye orodha ya wachezaji 23 walioorodheshwa kuwania tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka wa FIFA,na pengine wachache wanaweza kuhoji kuhusu kuwa mchezaji mwenye kiwango hicho kutoka barani Afrika kwa wakati huu.

Wakati yeye na wachezaji wenzake wa Klabu ya Manchester City wanaendelea kutafakari walivyopoteza taji la Ubingwa wa England dhidi ya Mahasimu wao Manchester United mapema mwaka huu,Yaya Toure ameuanza msimu huu akiwa kwenye kiwango cha juu akionyesha dhamira ya kurejesha taji hilo.