Sachin Tendulkar aaga Kriketi

Image caption Tendulkar anasemekana kuwa mchezaji bora zaidi wa Tennis duniani...lakini hiyo ni hoja inayoendelea kujadiliwa

Amepewa jina la 'maximum city' na mwandishi vitabu maarufu sana, huku mji wa Mumbai ukimuaga mchezaji kriketi mashuhuri zaidi nchini India.

Mchezaji bora zaidi wa Kriketi nchini India hii leo, ameondoka rasmi katika ukumbi wa mchezo huo, katika kile kinachosemekana kuwa mchezo wa lala salama wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, India itamenyana na West Indies katika mchuano wa mwisho wa Test katika uwanja mashuhuri wa Wankhede.

Huu ndio uwanja ambao mwaka 2011, Sachin Tendulkar aliweza kujionyesha kwa dunia kama mchezaji mashuhuri na hivyo nyota yake kuwakia hapa katika maisha yake kama mchezaji wa Kriketi kwa zaidi ya miaka 20 katika kombe la dunia la kriketi.

Neno 'maximum' hutumiwa wakati watu wanapomzungumzia mchezaji Sachin Tendulkar, natumai kumaanisha kuwa ameweza kufikia kilele cha mchezo wa kriketi.

Kwa mtu anayeshikilia rekodi ya kupata mikimbio mingi zaidi kwenye mchezo huo na kushinda kombe la dunia yamekuwa mafanikio na matarajio yake kama mchezaji muda huu wote.

Lakini ushindi huu ulikuwa jambo tofauti kwa Sachin Tendulkar kwa sababu aliweza kushinda kombe nyumbani kwao, yaani India.

Huu ni mji aliozaliwa Sachin na kulelewa katika familia ya kipato cha kadri, familia ya kawaida nchini India.

Awali,alizoea kucheza Soka na Tennis, Sachin alipelekwa na kakake katika uwanja maarufu wa kufanyia mazoezi ya Kriketi, wa Shivaji Park, akiwa na umri wa miaka 11 . Hakuwahi kamwe kujutia kwani hayo ndio yamekuwa maisha yake tangu hapo.

Alivunja rekodi zote katika michuano yote iliyofanyika nyumbani akiwa tu na umri wa miaka 16, Sachin Tendulkar alianza kuchezea timu ya taifa.

Rekodi na mikimbio nazo zikaanza kumiminika.

Image caption Tendulkar anashabikiwa na wadogo kwa wakubwa

Kwa mtu ambaye mikimbio zaidi ya wote kimataifa katika aina yote ya michezo ya Kriketi, alicheza kwa zaidi ya miaka 24 na kucheza mechi yake ya miambili na mechi ya Test ya mwisho mbele ya mashabiki wa nyumbani.

Hii pia ni idadi kubwa ya michuano ya Test ambayo imechezwa na mwanakriketi huyu.

Bodi ya kriketi ya India ambayo ndio ina fedha nyingi zaidi kuliko zote duniani, ina mipango mizuri kwa mchezaji huyu mashuhuri zaidi kuliko wote. Amepata tiketi 400 kwa mechi hii ya mwisho. Jamaa zake wote wanatarajiwa kufika katika mechi hii kumuona akicheza kwa mara yake ya mwisho.

Mamake anayeugua na ambaye anatumia kiti cha magurudumu, atakuwepo katika ukumbi wa wageni mashuhuri kumuona mwanawe akicheza kwa mara ya mwisho.

Kocha wake Ramakant Achrekar pia atakuwepo. Tiketi za kushudia mechi hiyo zenye picha ya Sachin Tendulkar, pia zimechapishwa ingawa watu wamekosoa namna zilizvyouzwa.

Wapenzi wa Kriketi mjini Mumbai, hawajafurahia sana kwani thuluthu mbili ya viti vya uwanja huo, vitatutumiwa na watu ambao hawakununua tiketi.

Wenye maduka mjini Mumbai, wanasubiri mauzo mengi, ya vifaa vilivyo na picha za Sachin huku vyumba vya kila hoteli iliyo kusini mwa Mumbai vikiwa vimekodiwa.

Mashabiki wa Kriketi nchini India, humtaja Sachin kama bingwa wa kriketi. Hata hivyo kuna mjadala kuhusu ikiwa yeye ndiye mchezaji bora zaidi wa kriketi duniani.