Walcott kurudi uwanjani?

Image caption Walcot amekuwa akiigua kwa kwaribu miezi miwili

Theo Walcott huenda akaichezea Arsenal siku ya jumaamosi ikiwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili baada ya kupona kutokana na majeruhi ya tumbo.

Walcott yumo katika kikosi cha kupambana na klabu yake ya zamani Southampton siku ya Jumaamosi.

Walcott mwenye umri wa miaka 24-aliumia katika pambano la ligi dhidi ya Stoke September 22 baada ya kutegua maumivu aliyopata katika pambano la siku nne zilizotangulia dhidi ya Marseille.

"hajachezea hata kikosi cha akiba lakini nitamjumuisha katika kikos ikamili cha Jumaamosi '' alisema kocha Arsene Wenger.

"yuko mzima kabisa."

Awali Wenger alimtumia Serge Gnabry kuchezea nafasi iliyoachwa na Walcott, lakini tangu wakati huo safu yake ya kiungo ilimaarishwa na kurejea kwa Mikel Arteta naJack Wilshere.

"Theo ana sifa tofauti na wachezaji wengine na nimefurahi sana kwamba amerejea" alisema Wenger