Arsenal yajiimarisha kwa mabao

Image caption Arsena iko mbele ya Chelsea kwa pointi nne

Bao la kwanza la mchezaji Nicklas Bendtner tangu Machi mwaka 2011, lilisaidia Arsenal kuicharaza Hull na kujiweka katika nafasi nzuri mbele ya washindani wao kwenye ligi ya Premier.

Bao la Bendtner lilitokana na mkwaju wa Carl Jenkinson huku Bendtner akisema kuwa limekuwa jambo gumu sana kwake kuona Arsenal wakipanda ngazi wakati wote akiwa mchezaji wa akiba.

Bao lengine liliingizwa na Mesut Ozil, kutokana na mkwaju wa Aaron Ramsey, na kufikisha mabao yao kuwa mawili kwa nunge katika dakika ya 47.

Mchezaji wa Hull, Jake Livermore nusura aingize bao lao la kwanza ingawa mlinda lango Wojciech Szczesny alilinyakua.

Meneja wa Hull, Steve Bruce, alisema kua halikuwa jambo la busara kuchezesha, washambululiaji wawili ili kutafuta pointi baada ya kupata ushindi wa ghafla dhidi ya Liverpool.

Arsenal sasa wana pointi nne mbele ya Chelsea huku wakiendelea kujizatiti katika kinyang'anyiro hiki cha kombe la Ligi ya Premier.