Arsenal 1 Everton 1

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsenal wanaongoza orodha ya pointi kwa alama tano

Klabu ya Arsenal imejinyakulia pointi moja baada ya kwenda sare ya bao moja dhidi ya Everton

Arsen Wenger aliwashirikisha wachezaji Jack Wilshere, Kieran Gibbs na Olivier Giroud baada ya kupumzishwa.

Gerard Deulofeu, iliipatia Everton nafasi ya kwenda sare na Arsenal huku ikiinyima Arsenal alama saba mbele ya mahasimu wake.

Deulofeu aliingiza bao hilo na kumaliza matumaini ya Arsenal ya kupata alama nyingine tatu mbele ya mahasimu wake licha ha Arsena kupata bao la Mesut Ozil.

Hata hivyo Arsenal inasalia kuwa mbele ya Liverpool kwa pointi tano.

Everton hata hivyo hawakuwa na wasiwasi wa mchezaji yeyote kuwa na jeraha.

Antolin Alcaraz alikuwa kwenye kikosi hicho lakini Leighton Baines, Arouna Kone na Darron Gibson walisalia nje.

Licha ya kuongoza orodha kwa pointi tano sasa, baadhi wana shauku ikiwa kweli Arsenal inaweza kushinda kombe la ligi la Premier,kwa sababu ushawishi wao kuweza kufanya hivyo bado haujawagusa mashabiki wengi wa soka.