Moyes :'Man U wako imara'

Image caption Moyes anasema Man U wanaweza kushinda mataji ila tu waboreshe mchezo wao

Meneja wa klabu ya Manchester United, David Moyes, amesema klabu hiyo ni miongoni mwa vilabu vitano bora zaidi vinavyoweza kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya lakini kinahitaji kujiboresha ikiwa kinataka kutimiza ndoto hiyo.

Klabu hiyo ambayo imeshinda kombe hilo mara tatu wameonekana kuchechemaa hasa baada ya kushindwa mara mbili mfululizo katika ligi ya Premier inayoendelea.

Man U wako juu kwenye orodha ya timu katika kundi A baada ya kuilaza Shakhtar Donetsk bao moja bila.

"nadhani tunaweza kushinda kombe hili,'' alisema Moyes.

"itatubidi kuimarisha mchezo wetu ili tuweze kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.Klabu kama Manchester United lazima iwe inajitahidi kushinda kombe hilo.''

Moyes ambaye alichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson msimu uliopita, alisema "lazima tucheze vyema wakati ,michuano hii ikiendelea.''

"ushindani ni mkali, lakini tutakwenda hatua kwa hatua.''

Phil Jones ndiye aliingiza bao la pekee dhidi ya Shakhtar wakati United iliepuka kuhindwa kwa mara ya tatu nyumbani kitu ambacho hakijawahi kufanyika tangu mwaka 1962. ''

Manchester iliposhindwa na Everton,Moyes alikosolewa sana lakini Jonny Evans akatetea wachezaji wenzake na kusema wamekosa tu kujiamini.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii