Manchester City yailima Arsenal

Manchester City na Arsenal
Image caption Manchester City na Arsenal

Manchester City imetoa ujumbe muhimu kwa wapinzani wao kwa kuinyuka Arsenal

Mechi hiyo ilikuwa ya kusisimua kutokana na wingi wa magoli yaliyoingia,jumla ya magoli 9.Manchester City ilimaliza kipindi cha kwanza ikiongoza kwa 2-1 kutokana na magoli yaliyofungwa na Aguero na Negredo.

Kwa kile kilichoonekana kupwaya kwa ngome za timu mbili,Manchester City iliongezea magoli zaidi katika kipindi cha pili kwa kuwatumia Fernandinho aliyefunga magoli 2,Silva na Yaya Toure aliyefunga goli la mwisho kwa njia ya penalty.

Upande wa Arsenal Theo Walcott alipachika mabao 2 na mlinzi Mertesacker akafunga goli la 3.

Ushindi huo wa Manchester City unawasaidia kupunguza pengo la alama tatu lililokuwepo kati ya timu mbili na kuonya Arsenal kuwa bado ina kazi ya kufanya licha ya kwendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 35.