Aboutrika soka basi sasa!

Klabu ya Al Ahly bado inatumai kuwa itaweza kumshawishi nyota wake Mohamed Aboutrika kuahirisha mipango yake ya kustaafu kwa mara nyingine.

Mchezaji huyo kiungo cha kati, aliondoka uwanjani akichechemaa katika mechi kati ya klabu hiyo na mabingwa wa Asia Guangzhou wakati wa kipindi cha mapumziko.

Guangzhou ilimaliza mechi kwa kushinda Al Ahly mabao 2-0 na kujipatia nafasi ya kukutana na Bayern Munich kwenye fainali ya klabu bingwa duniani.

Bila shaka sio hivyo ambavyo mashabiki wa soka Misri wangependa kumkumbuka Aboutrika mwenye umri wa miaka 35.

Aboutrika amekuwa kiungo muhimu katika soka ya Misri, kwa karibu miaka kumi na ameshinda ubingwa wa Afrika mara tano akichezea Ahly.

Kocha wa klabu hiyo hata hivyo ameelezea matumaini akisema kuwa wangali wanashauriana na Aboutrika,

Ameingiza mabao 14 katika mechi za Misri za kufuzu kwa kombe la dunia lakini hiyo haijatosheleza ndoto yake ya kutaka kucheza kwenye fainali.

Aboutrika, ambaye amesomea Filosofia pia anasifika kwa msimamo wake wa kisiasa pamoja na maswala ya kibinadamu.