Curbishley ajiunga na Fulham

Image caption Kipa wa Fulham

Alan Curbishley, ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya Fulham.

Kocha huyo wa zamani wa Charlton anarejea katika ligi kuu miaka mitano baada ya kufutwa kazi na klabu ya West Ham.

Curbishley mwenye umri wa miaka 56, ambaye alikisiwa kuwa huenda akateuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, anajumuika na Rene Meulensteen, ambaye alichukua mahala ka Martin Jol kama kocha wa Fulham mapema mwezi huu.

Meulensteen amesema Curbishley ana rekodu nzuri na anaelewa nini kinapaswa kufanyika ile wafanikwe.

Fulham wanachuana na Norwich tarehe siku ya alhamisi na kwa sasa wanashikilia nafasi ya kumi na tisa kwenye msururu wa ligi kuu ya premier.