Misri yapanda orodha ya FIFA

Haki miliki ya picha BBC World Service

Misri imepiga hatua kubwa zaidi miongoni mwa timu za Afrika katika orodha ya kwanza mwaka 2014 ya FIFA.

Imepanda alama kumi juu hadi katika nafasi ya 31 duniani.

Inamaanisha kuwa Misri ni ya nne katika ubora barani Afrika ikiwa juu ya taifa ya Nigeria walioshuka hadi nafasi ya saba.

Afrika Kusini ilipanda kwa alama nane na kushikilia nafasi ya 54 duniani hatua ambayo imeipelekea timu hiyo kuwa katika timu kumi bora zaidi Afrika.

Burkina Faso walishuka hadi nafasi ya 11 katika timu za Afrika.

Kwingineko hapakuwa na shughuli nyingi kwani ni mechi kumi na nane pekee za kirafiki zilichezwa tangu mwezi Disemba.

Hata hivyo, orodha itakayotolewa mwezi ujao, itazingatia matokeo kutoka katika mashindano ya kombe la taifa bingwa Afrika.

Fainali za mwaka huu zilihusisha klabau 16 ikiwemo Nigeria, Ghana na Afrika Kusini pamoja na Minnows kutMauka ritania.

Nchi kumi bora Afrika