Gedo arejea Al Ahly kutoka Hull

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Gedo alianza msimu wa pili na Hull mwezi Septemba

Mshambuliaji wa Misri, Gedo, amerejea katika klabu ya Al Ahly, baada ya klabu ya ligi ya Uingereza ya Hull kusitisha huduma za mchezaji huyo kwa klabu hiyo.

Gedo alikuwa anachezea Hull kwa mkopo.

Aidha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alianza msimu wake wa pili na Hull mwezi Septemba baada ya kuingiza mabao matano katika michezo 12 msimu uliopita.

Lakini alicheza tu mara tatu na kutumiwa kama mchezaji wa akiba mara mbili katika ligi hiyo.

Wakati Hull ilipowasajili Nikica Jelavic na Shane Long ,hapo ndipo huduma za Gedo zilipositishwa Hull.