Westbrom yatatiza Everton

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa Westbrom

Katika ligi kuu ya Premeir nchini England, Pepe Mel alianza kampeini yake kama meneja wa Westbrom kwa kuzoa alama moja pale timu yake ilipotoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Everton.

Kufuatia sare hiyo Everton imesalia katika nafasi ya tano na alama 42 ili hali Westron pia ikasalia katika nafasi yake ya kumi na mbili.

Kevin Mirallas alifungia bao na kuiweka Everton uongozini katika kipindi cha kwanza kabla ya Lugano kusawazisha dakika kumi na tano kabla ya mechi hiyo kumalizika.

Huku kocha huyo mpya akifurahia matokeo yake kocha wa Everton, Roberto Martinez amegadhabishwa na matokeo hayo.

Martinez amesema wachezaji wake walipoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza na kuwa kiwango chao kilishuka sana katika kipindi cha pili.

Wakati huo huo, wasimamizi wa mtandano wa Zoopla, wametangaza kuwa wamesitisha ufadhili wao kwa klabu ya Westbrom, kufuatia mzozo unaohusiana na madai ishara ya ubaguzi dhidi ya wayahudi, iliofanywa na mshambulizi wake Nicolas Anelka.

Anelka alionyesha ishara hiyo baada ya kufunga bao wiki tatu zilizopita.

Wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na makundi ya kiyahudi wanasema wanataka mchezaji huyo kupigwa marufuku, lakini klabu hiyo imekariri kuwa Anelka ana haki ya kuendelea kucheza.

Mel alimjumuisha Anelka katika kikosi chake kilichochuana na Everton, huku shirikisho la mchezo wa soka FA likiendelea na uchunguzi wake kuhusiana na sakata hiyo.