Manchester City yafuzu kwa fainali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji wa Manchester City Sergio Aquero

Manchester City imejikatia tikiti ya fainali ya kuwania ko be la ligi kwa mara ya kwanza, kwa zaidi ya miaka 38 baada ya kuilaza West Ham kwa jumla ya magoli tisa kwa bila.

Katika mechi ya raundi ya kwanza Manchester City iliinyuka West Ham sita bila kabla ya kuinyesha matatu zaidi siku ya Jumanne.

Negredo aliifungia City bao la kwanza na la pili kabla ya Sergio Aguero kuongeza la tatu.

Manchester City sasa itachuana na Manchester United au Sunderland katika fainali itakayogaragazwa katika uwanja wa wembley machi mbili

United wanawakaribisha Sunderland katika awamu ya nusu fainali ya pili siku ya Jumatano usiku, na watakuwa na kibarua kigumu kufuzu kwa fainali hizo baada ya kulazwa kwa magoli mawili kwa moja katika awamu ya kwanza.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Man City Manuel Pellegrini

Mapema mwezi huu kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini alisema kuwa watajaribu kushinda mataji yote manne wanayopigania kwa sasa, kombe la ligi kuu, FA, kombe la ligi na lile la klabu bingwa barani Ulaya.

Kwingineko mchezaji wa Westbrom, Nicolas Anelka anakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku ya kutoshiriki mechi tano mfululizo ikiwa atapatikana na hatia na shirikisho la mchezo wa soka nchini England kwa kuonyesha ishara ya ubaguzi.

Mchezaji huyo alifanya ishara hiyo inayotajwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya wayahudi baada ya kufunga bao dhidi ya westham tarehe 28 desemba mwaka uliopita.

Wadhamini wa klabu hiyo Zoopla wametangaza kuwa watasitisha ufadhili wao mwisho wa msimu huu kufuatia tukio hilo.