Chelsea yailaza Manchester City

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha Pellegrini wa Man City

Manchester City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza nyumbani kabla ya kukutana na Chelsea.

Kadhalika hii ndiyo imekuwa mara ya kwanza Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.

Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .

Kutokana na mechi hiyo Manchester City na Chelsea zina alama sawa lakini Mancity imefunga mabao mengi.

Liverpool iko katika nambari ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.