Laudrup afutwa kazi na Swansea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyekuwa kocha wa kilabu ya Swansea

Swansea City imemfuta kazi kocha wake Michael Laudrup na kumpa nahodha wa timu hiyo Garry Monk kuiongoza katika mechi ya ligi dhidi ya wapinzani wake Cardiff City Jumamosi ijayo.

Taarifa hizo zinajiri siku moja tu baada ya mwenyekiti wa kilabu hiyo Huw Jenkins kupuuzilia mbali tetesi kuwa walikuwa wamezungumzia mustakabali wa Laudrup.

Uvumi ulikuwa umesambaa kuhusu hatma ya Laudrup baada ya Swansea kushindwa kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa mara ya sita timu hiyo kupoteza katika mechi nane za Ligii kuu ya Uingereza na kuiacha na alama mbili tu juu ya timu ambazo zitateremshwa katika ligii hiyo.

Monk alikuwa amepigiwa debe kuchukua nafasi hiyo ikiwa mojawapo ya njia za kuboresha kikosi hicho.