Olimpiki ya msimu baridi yaanza Sochi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwenge wa Sochi

Mashindano yaliyo gharimu Kitita kikubwa zaidi katika historia ya Olimpiki yatafunguliwa Urusi leo huku medali 98 ziking'ang'aniwa katika siku kumi na sita.

Sochi, ambayo iko katika pwani ya Urusi itakuwa ukumbi wa takriban wanariadha 2,900 kutoka kote duniani wakishindana katika fani kumi na tano.

Maandalizi ya mashindano hayo yamekabiliwa na tishio uslama, wasiwasi kuhusu haki za binadamu mbali kucheleweshwa maandalizi.

Lakini kwa gharama ya kwa kima cha dola bilioni 30 za Marekani ,Sochi ndiyo michezo ghali zaidi kuwahi kuandaliwa katika historia ya mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi ikijumlishwa.

Canada, Norway Marekani ndizo nchi zinazopigia upatu kuongoza katika jedwali la Medali huko Sochi bila ya kuwasahau wenyeji wa mashindano hayo Urusi.

Uingereza inapania kushinda medali zisizopungua tatu za dhahabu.

Iwapo itafaulu basi itakuwa timu ya kwanza ya nchi hiyo kuandikisha matokeo bora katika mashindano hayo ya msimu wa baridi tangu mwaka 1936 .