Michezo ya Sochi yaanza Rasmi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufunguzi wa michezo ya Sochi ulikuwa wenye haiba kuu

Rais Vladmir Putin wa Urusi amefungua rasmi mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi katika mji wa utalii wa Socchi katika sherehe iliofana.

Waliokuwa wanariadha mashuhuri nchini Urusi waliubeba mwenge wa Olimpiki kabla ya kuwashwa na aliyekuwa mlinda lango wa mchezo ya magongo Vladislav Tretiak pamoja na Mchoraji wa barafu Irina Rodnina.

Awali mashabiki waliongozwa katika sherehe iliofana kuhusu historia ya Urusi na mchango wake ulimwenguni.

Katika siku 16 zijazo,karibia wanariadha 3000 watashiriki katika michezo 98 tofauti katika mashindano hayo yaliodaiwa kugharimu takriban dola billioni 50.